Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto, Ummy Mwalimu amewataka madaktari wazawa waliopo nchini kuomba nafasi za ajira ya udaktari nchini Kenya kwa mkataba maalum, ambapo ameeleza kuwa zoezi hilo limeanza rasmi Machi 18 mpaka Machi 27, mwaka huu wawe wameomba.

Waziri Ummy amesema kuwa waombaji ni wale watakaokidhi vigezo maalum ikiwemo asiwe katika utumishi wa Umma, Asiwe amejiliwa na mashirika ya umma ama mashirika teule ambayo yanalipiwa na Serikali.

Hayo ni kufuatia Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya kubainisha kuwa inatarajia kuwapeleka Madaktari wake waliopo nchini Tanzania kwenda kufanya kazi nchini Kenya kufuatia kuombwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenyatta.

Waziri Ummy ameeleza kuwa muombaji lazima awe amehitimu mafunzo ya “internalship” na mwisho awe amesajiliwa na baraza la Madaktari  nchini.

Amesema kuwa ajira hiyo itakuwa ni ya miaka miwili ambapo watapata mishahara na malupulupu mbalimbali katika ajira zao hizo huku akibainisha kuwa, jambo hilo ni jema na linaiingizia Taifa sifa kwa kupeleka wataalamu wake nje ya nchi kupata ajira.

Steve Nyerere: Nilitumia ujasiri wa kiume kuomba radhi hadharani
Mzimu wa CCM wazidi kumtesa Kingunge