Muimbaji kutoka Uganda Weasal, ametoa wimbo maalumu kwa ajili ya msanii Mowzey Redio, ikiwa ni sehemu ya kumbukumbu ya kifo cha msanii huyo aliyekuwa akishirikiana nae kimuziki kupitia kundi la Goodlife.
Wimbo huo wenye dakika nne umepewa jina la “Tokyayitaba’’ Weasal amesikika akitoa hisia zake kwa jinsi gani anamkumbuka na kumuenzi msanii huyo.
Weasal na Radio wamefanya kazi pamoja kwa miaka kumi kabla ya Radio kufariki dunia baada ya kupigwa na baunsa wa klabu ya usiku.
Weasal ambaye ni mdogo wa muimbaji nguli kutoka Uganda, Jose Chameleone ametumia Lugha ya Luganda na Kiswahili kwenye mashairi ya wimbo huo yanayoonesha uchungu alionao kufuatia kifo cha rafiki yake huyo.
-
Tanzia: Msanii Radio afariki dunia
-
Chameleone awatimua kwa panga waombolezaji msiba wa Radio
-
Aliyehusika mauaji ya Radio atiwa mbaroni
‘Kifo, Mungu alileta kifo, watu wanapotea kama upepo’’ hii ni sehemu ya mashairi ya Kiswahili yanayo patikana katika wimbo huo.
Radio alifariki February 1, 2018 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Case kufuatia majereha aliyoyapata baada ya kupigwa.