Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeandaa tamasha maalum la Mwezi wa Urithi kuenzi Utamaduni na Urithi wa Mtanzania lengo kubwa likiwa ni kunadi utalii, utamaduni, mila na desturi za makabila yote nchini ambayo ni zaidi ya 128.
Tamasha hilo limepanga kufanyika mwezi Septemba kila mwaka kuanzia mwaka huu 2018 na litajulikana kama Urithi Festival: Celebrating Our Heritage.
Aidha, Tamasha hilo linawalenga Watanzania wote nchini na waliopo ughaibuni, pia tamasha hilo litawashirikisha wadau wote wa utalii, utamaduni na Taasisi kutoka sekta binafsi, Mashirika ya Kimataifa, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, Vyombo vya habari, Taasisi za Elimu na Utafiti.