Ibada ya mazishi na baba na mwanae iliyofanyika Jumatano ya wiki hii nchini Uingereza iliingia doa kubwa la aibu baada ya moja kati ya runinga zilizokuwa zinaonesha tukio hilo kuonesha picha za video chafu za ngono.

Marehemu Simon Lewis mwenye umri wa miaka 33 na mwanae walifariki kutokana na  ajali mjini Cardif katika siku ya mkesha wa mwaka mpya.

Kiongozi wa Ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika katika eneo la kuchoma moto maiti la Cardiff Thornhill, Lionel Fanthorpe alilielezea tukio hilo kuwa tukio la aibu na lililokosea heshima waombolezaji waliokasirishwa sana.

“Nilikuwa naagalia waombolezaji badala ya kwenye Screen za TV, lakini niliposikia hizi kelele na waombolezaji wakielekea kwenye hiyo TV, niligundua kuna kitu hakiko sawa,” alisema Mchungaji Fanthorpe.

“Familia ya marehemu ilivunjiwa heshima, na baba mkwe wa marehemu Simon alikuwa amekasirishwa sana na kitendo kile,” aliongeza.

Mchungaji Cardiff Thornhill

Mchungaji Cardiff Thornhill

Mamlaka ya Cardif iliomba radhi kwa tukio hilo na kueleza kuwa runinga iliyoonesha tukio hilo ya Smart TV iliwekwa katika eneo hilo hivi karibuni, hivyo wanafanya uchunguzi kubaini chanzo cha video hiyo chafu kuonekana.

Msemaji wa Mamlaka ya Cardif aliviambia vyombo vya habari, “Tunafanya jitihada za kubaini iwapo runinga hiyo mpya ambayo ni ‘smart tv’ labda ilinasa picha hizo kwa bahati mbaya kupitia Bluetooth ama kupitia Wi-fi.”

 

Wema adai Zari anamchokonoa, aeleza kwa urefu bifu lao, uhusiano wake na Diamond, msikilize hapa
January Makamba: Uchaguzi wa Marudio Zanzibar ni Halali Kikatiba