Kamishna Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam, John Masimule, amesema kuwa Yusuph Manji atafikishwa Mahakamani kwa kosa la kuajiri wafanyakazi kutoka Nje ya Nchi na kuwaingiza kufanya kazi nchini bila kibali.
Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es salaam, amesema kuwa Manji atapelekwa mahakamani kwa kosa la kuingiza raia kutoka nchi za nje bila kufuata utaratibu na kanuni za sheria zinavyotaka.
Masimule ameongeza kuwa katika operesheni hiyo iliyoanza kufanyika katika Jiji la Dar es salaam, haijalishi mtu ana cheo gani wala uwezo wake wa kifedha kama ataenda kinyume na sheria atashughulikiwa kwa mujibu kwa sheria.