Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kiasi cha shilingi trilioni 7.87 kwa kipindi cha miezi sita iliyopita 2017/2018.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma na elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa katika mwezi Desemba pekee TRA imekusanya kiasi cha shilingi trilioni 1.66 ikilinganishwa na mwezi Desemba 2016.
Aidha, TRA imewasisitiza wananchi kulipa kodi kwa muda ili iweze kufikia malengo iliyojiwekea katika kuleta maendeleo.
Hata hivyo, Kayombo ameongeza kuwa TRA imeanza kufanya kampeni kubwa kwa nchi nzima ya kusajili walipa kodi ili kuondoa changamoto zilizokuwepo.