Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kumtangaza raia kwenda kituo cha polisi bila kufuata utaratibu.
Amesema kuwa Mbowe amefanya maamuzi mazuri kutokwenda kituo cha polisi, kwani taratibu za kisheria hazijafuatwa.
Aidha, Zitto ameongeza kuwa kama Mbowe angekuwa anahusika na madawa ya kulevya, basi yeye angekuwa punda wake kwa kubeba mizigo ya unga kwani ndiye aliyemuibua katika siasa akiwa chuo kikuu.
“Kitendo hicho cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ni cha kulaaniwa si tu na wanasiasa,ni pamoja na wananchi wote kwani kitendo hicho ni cha udharirishaji,”amesema Zitto.
.