Kiongozi wa ACT- Wazalendo na mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa mfumo wa kodi ya kimataifa haujafuatwa hivyo Tanzania haiwezi kuwadhibiti wawekezaji wa uchimbaji wa madini.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Paramagamba Kabudi anajua kinachoendelea.

Aidha, Zitto amemtaka waziri huyo kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu kile kinachoendelea kati ya serikali na kampuni hiyo ya uchimbaji madini kwakuwa sheria za kimataifa anazifahamu.

“Nchi za wenzetu wamesaini mfumo wa kodi wa mikataba ya kimataifa, ndiyo maana wanapata faida kubwa, lakini haya yote Prof. Kabudi anafahamu yote haya, hapa tumepigwa changa la macho hapa,”amesema Kabwe

Beka Flavour 'aikataa' Yamoto Band
Korea Kaskazini yaapa kutositisha mpango wa silaha za nyuklia