Kiongozi wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa watafungua kesi mahakamani kupinga baadhi ya vifungu vilivyomo katika Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 ambayo amedai inanyima uhuru wa wananchi kuchambua takwimu.
Ameyasema hayo hii leo wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya kitengo cha upelelezi wa makosa ya kifedha jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kuwa haiwezekani kukawa na mamlaka moja ya kutoa takwimu.
“Tunataka kufungua kesi mahakamani kupinga sheria ya takwimu kuzuia watu kuchambua, huko ndiko ukweli utajulikana na wananchi watajua sheria hii ilivyo. Hii itakuwa kesi ya kwanza kwa sheria hii kupelekwa mahakamani,” amesema Zitto.