Mtandao wa ZOOM Tanzania na Brightermonday wamefungua milango kwa wahitimu wa vyuo vikuu kwa kuwasaidia kupata ajira.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Masoko kutoka ZOOM Tanzania na Brightermonday, Elisha Simon katika hafla ya uzinduzi wa mfumo utakaowasaidia wahitimu hao kufikia malengo yao.
Amesema kuwa mfumo huo uliozinduliwa ni mzuri na ni msaada mkubwa kwa wahitimu kuweza kujua maendeleo ya maombi yao ya kazi.
Aidha, Elisha amesema kuwa mfumo huo unawawezesha pia wa ajiri kutangaza nafasi za kazi kuwafikia watu wengi zaidi kwa wakati mfupi.
“Tumefanya kongamano hili kwa ajiri ya kuwasaidia wahitimu wa vyuo, maana kwasasa wamekuwa wakihangaika sana kuhusu masuala ya ajira,”amesema Simon
-
Wabunge wapinga uendeshwaji kampeni ya Makonda
-
Serikali kujenga makumbusho ya marais wastaafu
-
Ndugai adai Bunge haliwezi kuidhinisha fedha za matibabu ya Lissu