Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kupitia virusi viitwavyo HBV (Hepatitis B Virus), ambavyo vikiingia mwilini hushambulia ini. Ni moja kati ya magonjwa hatari zaidi na hupoteza maisha ya watu wengi kwa muda mfupi.

Dar24 ilimtafuta ‘Daktari’ wa magonjwa ya binadamu, Romana Malikusemo wa Hospitali ya TMH iliyopo Sinza jijini Dar es salaam, ambaye ameelezea kwa kina juu ya ugonjwa huo.

Dk. Romana amesema watu wanaoishi na ukimwi wanaweza kuishi hata miaka 50 lakini Hepatitis B endapo itakuta ini tayari limeshambuliwa vibaya au afya haikuwa nzuri mtu anaweza kupoteza maisha katika muda mfupi sana. Hivyo, Hepatitis B ina makali zaidi na ina uwezo mkubwa wa kufanya mtu apoteze maisha haraka zaidi kuliko Ukimwi.

Tazama video hapa chini Daktari akielezea namna ambavyo ugonjwa unaweza kushambulia ini, dalili zake, kinga na kwa nini hakuna tiba.

Rungwe aripoti Polisi - Osterbay
Video: Mjamzito alivyotoboa tumbo na kutoa mtoto, Askofu wa KKKT amuangukia JPM