Mmoja wa mashahidi katika kesi inayomkabili mshukiwa wa ugaidi, Mhubiri tata Paul Mackenzie, ameieleza Mahakama nchini Kenya kuwa wafuasi wote walitakiwa kufunga isipokuwa familia ya Mackenzie.
Shahidi huyo (17), amesema familia ya Mackenzie wenyewe walikuwa wakila na kunywa na walisema wangefunga kioindi ambapo wafuasi wote wangekuwa tauari wameshafariki.
Mhubiri huyo tata Paul Mackenzie, anadaiwa kuwalazimisha Waumini wake kuanzia Watoto wadogo hadi Watu wazima kufunga kula na kunywa hadi umauti kama njia ya moja kwa moja ya kufika kwa Mbinguni.
Alifikishwa Mahakamani kwa mara ya kwanza Aprili 17, 2023 na mara kadhaa amekuwa akifanya vituko kwa kugoma kula au kuwafai Waandiahi wa Habari mgao wake akidai wameingiza pesa nyingi kwa kuandika habari zake.