Idadi ya watu waliokufa duniani kutokana na ugonjwa wa COVID-19 imepindukia milioni tatu kufikia Jumamosi, licha ya kampeni ya chanjo dhidi ya ugonjwa huo kuendelea kushika kasi.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la Ufaransa, AFP zaidi ya vifo 12,000 duniani kote viliripotiwa kila siku katika muda wa wiki moja iliyopita na kupindukia vifo milioni tatu kufikia Jumamosi.

Janga hilo halijaonyesha dalili ya kupunguza makali yake, huku watu 829,596 wakiambukizwa virusi vya corona siku ya Ijumaa pekee, idadi hiyo ikiwa ya juu zaidi kwa watu kuambukizwa kwa siku moja.

Mji mkuu wa India, New Delhi siku ya Jumamosi ulizifunga shughuli zake za umma baada ya kurekodi visa vipya 234 vya corona pamoja na vifo 1,341.

Mbio za ufungaji bora VPL, Kagere amtaja Dube
Waziri Mkuu atumbua UDART