Takwimu za utafiti mpya zilizochapishwa katika jarida la AAP Pediatrics na Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa na Chuo cha Marekani cha Madaktari wa Watoto, umesema Vifo vya watoto vinavyotokana na Bunduki nchini humo vimefikia kiwango cha juu zaidi
Utafiti huo, ulibainisha kuwa watoto 4,752 walikufa kutokana na majeraha yanayohusiana na bunduki mwaka wa 2021, kutoka vifo 4,368 vya mwaka wa 2020 na 3,390, kwa mwaka 2019 huku Vurugu zinazohusishwa na bunduki zimekuwa sababu namba 1 ya vifo vya watoto tangu mwaka 2020.
Utafiti huo, pia ulichapishwa huku Wabunge wa Jimbo la Tennessee wakifungua kikao maalum kuhusu usalama wa umma, baada ya shambulizi la risasi katika shule ya Nashville mapema mwaka huu, lililowaua watoto watatu na walimu watatu.
Daktari wa watoto wa Carolina Kusini na mtafiti wa kuzuia mashambulizi ya kutumia bunduki, Annie Andrews ambaye hakuhusika katika uchunguzi huo, alisema kwamba alipokuwa Daktari hakudhani kamwe kwamba angetunza watoto wengi wenye majeraha ya risasi.