Vilio, simanzi na vifo vinazidi kutikisa katika mji mkuu wa Sudan Khartoum, baada ya milio ya mizinga na maroketi kusikika, saa chache baada ya shambulio la anga katika eneo la kusini mwa jiji hilo na kuwaua watu 22 wakiwemo watoto wawili.

Kwa mujibu wa kundi moja la wanaharakati wa Sudan, ambalo lilikuwa ni miongoni mwa makundi yaliyoandaa maandamano ya kudai demokrasia na kutoa usaidizi kwa familia, limesema shambulio hilo limetokana na mapigano baina ya Makamanda wawili wanaogombania Madaraka.

Awali, Wanaharakati hao walionya kwamba vifo vingi vimekuwa havijarekodiwa, kwani miili ya wahanga haikuweza kupelekwa Hospitali kwani watu wengi waliungua na moto au kukatika vipande katika mlipuko huo.

Kwa mujibu wa Taasisi zinazofuatilia mzozo huo na kuhifadhi data, zimesema tangu kuuanza kwa vita hiyo baina ya Jeshi la Serikali na kikosi cha Wanamgambo wa akiba wa RSF katikati ya Aprili 2023, watu wapatao 5,000 wameuawa.

Bernard Morrison alamba mkataba wa masharti
Robertinho aikaribisha Al Ahly