Serikali nchini, imekemea vitendo vya baadhi ya Wafanyabiashara wachache wasio waaminifu wanaoendelea kuingiza, kuzalisha na kusambaza bidhaa za plastiki zisizokidhi viwango zinazotumika kama vifungashio ambazo zimekuwa chachu ya uchafuzi wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini.
Akizungumza katika zoezi la usafi wa mazingira katika kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Jijini Dodoma Naibu Waziri wa Kilimo, Antony Mavunde amesema ni wajibu wa Wafanyabiashara kushirikiana na taasisi za Serikali katika kusimamia usitishaji wa Matumizi ya bidhaa za plastiki.
Amesema, “kumekuwa na juhudi mbalimbali za Serikali na wadau katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira utokanao na taka za plastiki, hata hivyo bado kuna ukwiukwaji wa sharia kwa baadhi ya Wafanyabiashara wanaoingia na kuzalisha mifuko ya plastiki isiyokidhi viwango ambayo inayotumika madukani na watoa huduma.”
Mavunde pia ametaka Wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali katika kudhibiti matumizi ya mifuko na bidhaa za plastiki kwa kutoa ushirikiano kwa viongozi wa serikali za mitaaa ili kkurahisisha zoezi hilo la kutokomeza vifungashio visivyokidhi viwango ambavyo vimekuwa visambazwa kupitia njia za panya.