Baada ya matokeo ya michezo ya usiku wa kuamkia leo katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa mambo yanaelekea kuwa matamu kutokana na timu zitakazocheza hatua ya mtoano ya michuano hiyo kujulikana.

Michuano hiyo itakayoendelea tena mwezi Februari mwakani, inaingia katika hatua ya mtono (16 bora) na droo ya ratiba ya hatua hiyo itapangwa kwa kuzingatia kanuni ya timu zilizomaliza nafasi ya kwanza katika kila kundi dhidi ya timu zilizoshika nafasi ya pili.

Kutokana na muongozo wa kanuni hiyo kuna wasi wasi mkubwa kwa mabingwa watetezi Real Madrid waliomaliza katika nafasi ya pili, wakakutana na mmoja wa vigogo wa soka barani hyumo,jamboa mbalo linasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kote.

Vigogo wengine waliomaliza katika nafasi ya pili ni FC Bayern Munich, Juventus na Chelsea.

Hafla ya upangaji wa michezo ya hatua ya mtoano (16 bora), itafanyika Desemba 11 makao makuu ya shirikisho la soka barani Ulaya yaliopo mjini Nyon nchini Uswiz.

Timu zilizomaliza katika nafasi ya kwanza katika makundi yote manane.

Manchester United

Paris Saint-Germain

AS Roma

FC Barcelona

Liverpool

Manchester City

Beşiktaş

Tottenham Hotspur

Timu zilizomaliza katika nafasi ya pili katika makundi yote manane.

FC Basel

FC Bayern Munich

Chelsea

Juventus

Sevilla

Shakhtar Donetsk

FC Porto

Real Madrid

Mchoro wa picha ya Yesu waelekea Abu Dhabi
Trump afanya maamuzi magumu kuhusu mji wa Jerusalem