Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaita viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa ili wazungumzie utekelezaji wa sheria zinazosimamiwa na ofisi hiyo.

Taarifa  toka  ofisi hiyo kwa Makatibu Wakuu wa Vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu, imeeleza kuwa kikao hicho cha

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza kikao hicho kitaanza saa 2 asubuhi , Oktoba 2 jijini Dar es Salaam

.“Washiriki watakuwa ni Mwenyekiti wa Taifa na Katibu Mkuu, mnaombwa kuhudhuria bila kukosa” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa kwa niaba ya Msajili wa Vyama Vya Siasa.

Hivi karibuni Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilikiandikia barua Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu kitendo cha kumnadi Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif,  ofisi ya msajili imekaliliwa ikisema jambo hilo ni kinyume cha sheria.

Ofisi hiyo ilieleza kuwa kwa sasa hakuna chama chochote cha siasa, kinachoweza kushirikiana katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu ; na endapo kitafanya hivyo kitafanya kosa la kisheria.

Nyahoza alisema kutokana na kosa kama hilo, tayari ofisi ya msajili imekiandikia Chadema barua ya kukitaka kujieleza kwa kitendo chake cha kumnadi Maalim Seif huko Zanzibar na pia kumnadi Zitto huko Kigoma.

28 mbaroni kwa uhamiaji haramu
Watano wauawa katika shambulio la roketi -Baghdad