Scolastica Msewa, Kibaha – Pwani.
Chama cha Kikomunisti cha nchini China – CPC, kimetoa ufadhili wa mafunzo mafupi ya siku kumi kwa wanachama 50 wa Chama Cha Mapinduzi – CCM (Umoja wa Vijana na UWT), waliochaguliwa kote nchini ili kuwajengea uwezo masuala ya Siasa, Uchumi na mkakati wa kuendeleza mahusiano kati ya China na Tanzania.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo katika Shule ya Uongozi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kibaha mkoani Pwani, Naibu Katibu Mkuu CCM Bara, Anamringi Macha amesema ni mahsusi kwa ajili ya kuwajengea uwezo Viongozi, ili na wao waweze kwenda kutoa elimu baada ya kuhitimu.
Amesema, Viongozi hao watapata fursa ya kupewa mafunzo hayo kupitia wawezeshaji Viongozi Wasomi wabobezi na wanazuoni ambao ni viongozi wakongwe katika historia ya nchi kwa kufanya kazi kwa miaka mingi serikalini ili wawafundishe viongozi hao uvumilivu katika kulitumikia taifa.
Amewataja Wawezeshaji hao kuwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa na Katibu Mkuu kwa kipindi cha miaka kumi,pia alikua Mkuu wa Chuo Cha CCM Kivukoni Kivukoni Mzee Philip Makula, Komredi Stephen Wassira, alikuwa Naibu Katibu Mkuu Visiwani CDE Abdallah Mabodi, Prof. Samuel Wangwe , Prof. Paramagamba Kabudi na Kanali Mstaafu Simbakalia.