Uongozi wa jamii ya Kwazulu Natal, Afrika Kusini, imewataka wanaume ambao wana umri wa kuoa kulipa kodi, na kuwa na barua ya utambulisho wa umiliki wa makazi.

Katika taarifa iliyoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari nchini humo, imeeleza kuwa kodi hiyo ambayo inagharimu Randi 50 ya Afrika Kusini ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi 8,200 za Tanzania, wanatakiwa kulipa kila mwezi.

Kitendo hicho kimeanza kulalamikiwa na watu wengi wakiwemo wazazi wa vijana ambao hawajaoa na hawana kazi, kwani wao ndio hulazimika kuwalipia kodi hizo.

“Wanalipa kodi, ingawa hawajaoa, nililipa kwa kijana wangu wa kwanza, na wapili akafika miaka 18, nikapaswa kumtafutia barua ya umiliki wa makazi na kulipa, wa tatu ambaye naye anaingia miaka 18 naye hajaoa na yuko Johanesburg anatafuta kazi,”amesema mmoja wa wazazi Busisiwe Mthembu

Hata hivyo, kiongozi wa eneo hilo Thathezakhe Ngobese, amesema kuwa kodi hiyo siyo kwa ajili ya kulisha familia yake, bali hutumika kusaidia matumizi madogo madogo kwenye uongozi wao ikiwemo mahakama za kijamii, wanaofanya usafi maeneo hayo na mengineyo.

 

Waziri Mkuu akutana na makamu mwenyekiti wa bunge la China
Serikali yawatahadharisha Wahasibu