WACHEZAJI kadhaa wa kikosi cha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 23 wameitwa katika kikosi cha wakubwa cha Nigeria kwa ajili ya mechi dhidi ya Tanzania mwezi ujao kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika.
Kocha mpya, Sunday Oliseh amewajumuisha kikosini Stanley Amuzie anayecheza Italia, Nahodha wa FC Taraba, Usman Mohammed, Oghenekaro Etebo wa Warri Wolves na kiungo wa Enyimba, Kingsley Sokari.
Beki wa kushoto, Amuzie, ambaye ni hivi karibuni amehamia Italian katika timu ya Serie A, Sampdoria, alimvutia kocha huyo mapema mwezi huu katika ushindi wa U23 wa 2-1 dhidi ya Kongo mjini Port Harcourt.
Wachezaji wa ndani wa Nigeria wanaotarajiwa kuwamo kikosi cha Eagles wataingia kambini wakati wowote kuanzia sasa.

Twiga Stars Yaelekea Zanzibar
Chenge Akiri Kupokea Fedha Za Escrow, Apangua Gia Ya Sakata La IPTL