Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Ajira, Kazi Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema anashindwa kujenga hoja, ili iongezwe fedha katika mfuko wa maendeleo ya Vijana kwa kuwa fedha wanayopewa na Serikali kupitia mikopo matokeo yake hayaonekani.
Mhandisi Luhemeja ameyasema hayo akiwa Babati Mkoani Manyara, na kuongeza kuwa ili Vijana waweze kuaminiwa na kuwezeshwa na Serikali Ofisi ya Waziri Wkuu inaenda kutengeneza kanzi data Nchi nzima, ili kuwatambua na kuwaunganisha na fursa.
“Ofisi ya Waziri Mkuu inasimamia mafunzo ya uanajenzi ili Vijana wapate ujuzi, tutaziomba Wizara inapotangaza kazi waseme kwa Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya, ili ziwasaidie Vijana kupata kazi. Programu ya Build Better Tomorrow (BBT) iliyoanzishwa na Serikali nayo inawasaidia Vijana kunenepesha Ng’ombe na kufanya kilimo cha kisasa.”
Aidha, Lumeleja pia aliwataka vijana kufanya kazi kwa umoja waungane ili muweze kufanya kazi za maendeleokwani uzoefu unapatikana kwa vitendo huku akisema magroup ya Whatsapp waliyonayo yasiwe ya vibonzo bali yawe ya kupeana taarifa za fursa mbalimbali.
Amesema, Ofisi ya Waziri Mkuu imefanya utafiti ambao unaonesha Vijana wapo milioni 25 Nchi nzima na milioni 14 ndio nguvu kazi huku asilimia 25 wakiwa na ukosefu wa ajira, asilimia 18 wanakosa ajira, asilimia 15 wanakosa ujuzi na elimu na asilimia 5.6 kukosa uzoefu.
Naye Dkt. Chris Mahoki kutoka Chuo kikuu cha Dar es salaam, alisema kiwango cha Wasichana kuwaamini Vijana wa kiume imeshuka kwani wanaogopwa na watu ambao hawataki kukutana wakiogopa kuibiwa na akina mama wanawaogopa Vijana ili wasiweze kuwabaka huku mchokoza mada, Felix Mlaki akisema Vijana wanatakiwa kujitambua kwani wao kwa asilimia 70 ndio nguvu kazi ya Taifa.