Vijana wilayani Ruagwa wameipongeza Serikali kwa kuwawezesha kupata mafunzo ya kilimo cha Kisasa kwa kutumia teknolojia ya kitalu nyumba (Greenhouse) ambayo yamekuwa ni chachu kwao kujikwamua kiuchumi.

Pongezi hizo zimetolewa jana wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alipotembelea vijana hao katika Kijiji cha Chimbila “A” kilichopo Wilaya ya Ruagwa kukagua maendeleo ya mafunzo waliyopata vijana kupitia teknolojia ya Kitalu Nyumba

Mhagama alieleza kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imeonesha kuwajali, kuwatambua na kuwathamini vijana kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yamekuwa yakiwasaidia sana katika kuwaendeleza vijana kulima kwa mkakati.

“Mafunzo hayo yamewajengea uwezo vijana kushiriki kwa wingi kwenye kilimo cha aina hii kwa kuwa kinatija na ufanisi, hivyo vijana watakuwa wanapata mavuno zaidi katika eneo dogo kuliko eneo la wazi, uwezo wa kupata soko la mazao utakuwa wa uhakika, matumizi ya maji ni madogo katika kilimo hicho na hudhibiti viwatilifu,” amesema Mhagama

Ameeleza kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ilianzisha Programu ya Ukuzaji Ujuzi ikiwemo mafunzo hayo ya kilimo cha Kisasa ikiwa ni mkakati wa serikali baada ya kubaini asilimia 56 ya nguvukazi nchini ambao ni vijana wamekuwa na changamoto ya ajira.

Aidha amewasihi vijana kuendelea kutunza vitalu nyumba hivyo kwa kuwa watanufaika kiuchumi na sambamba na kuwaleta maendeleo yao na jamii kwa ujumla.

Baadhi ya vijana walionufaika na mradi huo akiwemo Lucas Mwindima amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imeonesha dhamira ya dhati katika kuwawezesha vijana wanapata ujuzi utakaowawezesha kukuza ujuzi wao na kuwaondoa katika hali ya umaskini.

Katika kupongeza jitihada hizo wanufaika wa programu ya kilimo hicho walibainisha mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata ujuzi wa kilimo cha mazao biashara pamoja na ongezeko la ajira kwa vijana waliowezeshwa elimu hiyo.

Pia Waziri Mhagama alitembelea kikundi cha Ruangwa Materials ambacho kimenufaika na Mkopo wa Maendeleo ya Vijana unaoratibiwa na Ofisi yake kupitia Idara ya Manedleo ya Vijana.

Serikali yaagiza wafugaji kuunga mkono uhamilishaji Mifugo
Waziri Mkuu wa Ethiopia ashinda tuzo ya amani ya Nobel, kukabidhiwa Sh 20 bilioni