Mahakama ya Haki za Kibinadamu ya Ulaya, inatarajia leo Septemba 27, 2023 itachunguza malalamiko ya Vijana sita wa Ureno, ambao kwa mara ya kwanza wamezishtaki nchi 32 kwa kutochukua hatua za athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Vijana hao, wenye umri katibya miaka 11 hadi 24, wanadai walipata wazo la kuzishtaki nchi hizo baada ya kufuatilia kwa karibu ajali ya moto, ambao uliteketeza maelfu ya hekta za misitu na Kahana, hivyo kusababisha vifo vya zaidi ya watu 100 nchini mwao mwaka 2017.

Picha kwa hisani ya (Photo by Ami Vitale)

Wamesema, maafa hayo yaliwafanya kufahamu juu ya ongezeko la joto duniani, tabia nchi, na hamu kubwa ya kudai uwajibikaji kutokana na mataifa hayo kutochukua hatua zozote stahiki na hivyo kuona kama ni tukio la kawaida ilhali lilisababishwa na shughuli za kibinadamu ambazo zingeweza kusimamiwa.

Mmoja wa Vijqna hao, Claudia Duarte Agostinho, qkiwa na dada yake, kaka yake, jirani yake na marafiki zake wawili, alisema siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa muda mrefu hatimaye imewadia, ikiwa ni Miaka sita baada ya kuanza hatua zao za kisheria.

Miquissone awekewa mpango maalum Simba
Zungumzeni na jamii kukomesha unyanyasaji - Dkt. Biteko