Wananchi hasa Vijana wametakiwa kutumia vyema fursa ya uwekezaji katika kilimo, ili kujitengenezea ajira ya kudumu, kipato na kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa zima kiujumla.

Wito huo, umetolewa na Spika wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya, Dkt. Tulia Ackson wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji nanenane, yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.

Dkt. Tulia (wa tatu kushoto), akicheza na Wasanii wa Burudani wakati alipotembelea maonesho hayo ya Kilimo nanenane jijini Mbeya

Amesema, “Serikali yetu imejitahidi kuwekeza na kuwawezesha vijana kujikita katika kilimo ikiwemo uanzishwaji wa mradi wa mashamba makubwa ya kuwezesha vijana kulima kibiashara, hakuna budi kila mmoja kuona ipo tija ya kushiriki katika uwekezaji huu.”

Aidha, Dkt. Tulia meongeza kuwa ni wajibu wa kila Mwananchi kuungana na Serikali katika kutimiza azma ya kufanikisha mapinduzi ya kilimo nchini, ili kuleta matokeo chanya na kumkomboa Mkulima.

Uwekezaji wapunguza matumizi uagizaji Sukari nje
Kijana akata rufaa abadili jina la ukoo kukwepa ulevi