Ofisi ya Makamu wa Rais, imeendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya Muungano na Mazingira katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa, yanayofanyika Babati Mkoani Manyara, yanayokwenda sambamba na uzimwaji wa Mwenge wa Uhuru, Oktoba 14, 2023.

Akitoa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hilo, Afisa Elimu Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Martha Ngalowera amesema Vijana wanaweza kujipatia kipato kwa kuangalia fursa mbalimbali za utunzaji wa mazingira zinazopatikana katika eneo analoishi.

Afisa Elimu Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Martha Ngalowera akitoa elimu ya Muungano na Mazingira kwa wananchi waliotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa inayofanyika Babati, Mkoani Manyara.

Amesema, “mazingira yanatoa fursa nyingi kwa vijana kama vile upandaji wa miti wa matunda unavuna matunda na kujipatia fedha lakini hata miti yenyewe ni biashara kubwa, utunzaji wa taka unaweza ukazalisha mbolea na ikatumika na watu wengi katika mashamba.”

Kwa upande wake Mhandisi Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Onespholy Kamukuru amesema lengo la uwepo wao katika ‘Wiki ya Vijana’ ni kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira.

Watafiti wasaidie ufumbuzi changamoto za Mazingira - Jafo
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Oktoba 12, 2023