Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema hatima ya wabunge waliokata rufani baadaya kuvuliwa uanachama wa chama hicho, itajulikana baada ya kuketikwa vikao stahiki vya chama hicho.

Amesema kuwa baada ya wabunge hao kukata rufani, wanaamini kwamba uongozi wa juu wa chama hichoutakapoketi kwa ajili ya kuamua hatima yao, utatenda haki kwa kila mtu.

“Chama chetu bila kuwahusisha viongozi wa chama na bila uamuzi wa chama, mama na dada zetu waliapishwa katika mazingira ya kutatanisha na bila kuidhinishwa na chama. Walikata rufani.

Vikao stahiki vya chama vitakaa wakati mwafaka na kusikiliza rufani zao na nina hakika, haki itatendeka,” amesema Mbowe.

Akizungumzia ushirika kati ya chama hicho na ACT-Wazalendo, Mbowe amesema walikubaliana kwa pamoja kuupingauchaguzi huo, lakini hawakushirikishwa katika uamuzi mwingine ulioendelea ikiwamo kuunda serikali ya umoja wakitaifa visiwani Zanzibar.

“Tulisaini tamko lenye msimamo wa pamoja makao makuu ya CHADEMA Oktoba 31 mwaka jana na hicho ndiyo kilikuwa kikao cha mwisho, mengine yaliyofuata hatukushirikishwa,” amesema Mbowe.

Ujerumani yachukua hatua kali za kupambana na corona
Majaliwa: Vijana mna fursa ya ajira Nyasa