Vilio na simanzi vimetawala katika ofisi za makao makuu ya kampuni ya Azam TV ambapo wafanyakazi watano wa kampuni hiyo wanaagwa baada ya kufariki kwenye ajali ya barabarani.

Ajali hiyo iliyotokea mkoani Singida na iligharimu maisha ya wafanyakazi hao watano waliokuwa wakielekea wilayani Chato mkoa wa Geita kwaajili ya shuguli ya TANAPA.

Aidha, gari aina ya Coaster iliyokuwa imewabeba wafanyakazi hao iligongana uso kwa uso na lori, ambapo watu wengine wawili ambao si wafanyakazi wa Azam Media nao walifariki dunia.

Wafanyakazi wa Azam TV waliofariki kwenye ajali hiyo ni Salim Mhando (muongozaji wa matangazo), Florence Ndibalema (Mhandisi wa Sauti), Sylvanus Kasongo (Mhandisi Mitambo) na wapiga picha wawili Said Haji na Charles Wandwi.

 

ICC yamkuta na hatia ya mauaji, ubakaji aliyekuwa Mkuu wa Majeshi
LIVE CHATO : Rais John Pombe Magufuli akizindua hifadhi mpya ya Taifa ya Burigi