vinara wa ligi ya nchini Hispania  Atletico Madrid wameonyesha nia ya kutaka kumrejesha kundini mshambuliaji wake wa zamani, Diego Costa.

Rais wa Atletico Madrid, Enrique Cerezo ameripotiwa kuwa na kikao cha mara kwa mara na baadhi ya viongozi wa benchi la ufundi kwa ajili ya kupanga mikakati ya kusuka kikosi hicho ikiwemo kumnasa mkali huyo.

Baadhi ya viongozi wameonekana kuunga mkono mpango wa kutaka kurejea kwa mchezaji huyo ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea.

Mchezaji huyo mwenye asili ya Brazil lakini ana uraia wa Hispania, aliuzwa Chelsea kwa pauni mil. 32 mwaka jana akitia saini mkataba wa miaka mitano.

Costa akawa msaada mkubwa kwa Chelsea ambapo aliweza kuisaidia timu hiyo kutwa ubingwa wa England na Kombe la Capital One katika msimu wake wa kwanza.

“Hivi sasa ni mapema mno kusema chochote kuhusu Diego, ni mchezaji wa Chelsea na anaangalia mstakabali wake katika klabu yake,” alisema rais huyo.

Ufalme Wa Soka La England Wapelekwa Emirates Stadium
Azam FC Wanatazamwa Kama Silaha Kwa Yanga