Uongozi wa timu ya Manchester City umeandaa mechi ya kumuaga rasmi nahodha wao wa zamani Vincent Kompany ambayo itapigwa siku ya Jumatano usiku .

Mechi hiyo itakutanisha baina ya magwiji wa timu hiyo dhidi ya nyota wa zamani wa Ligi kuu ya Uingereza ambapo kikosi cha City kitakuwa chini ya kocha Pep Guardiola huku cha Ligi kuu chini ya Roberto Martinez.

Kompany amemtaja Leroy Sane kama mchezaji anaye mtamani kumuona  akichuana na aliyekua beki nguli enzi za soka lake ambaye ni Gary Neville ili wachuane uwanjani.

” Bahati mbaya Sane ameumia nilitaka kumuweka upande wa Nevile nilitaka kutamfuta mchezaji mwenye kasi zaidi acheze dhidi ya Neville labda rafiki yangu akajifiche kwenye nafasi ya beki wa kati ”

Kocha Simba: Tunatoka na ushindi kwa Mtibwa
Ujumbe wa Makonda, Jokate baada ya Nape kumuomba msamaha Rais Magufuli