Kiungo Mshambuliaji ‘Winga’ wa Real Madrid, Vinicius Jr anaweza kuwa nje ya uwanja kwa muda wa hadi wa majuma sita kutokana na kusumbuliwa na misuli ya paja.

Nyota huyo alipata tatizo hilo juma lililopita katika mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Celta Vigo, ambao Real Madrid iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa Balaidos nchini Hispania, Vinicius Jr alitolewa katika dakika ya 18 na nafasi yake kuchukuliwa na Joselu.

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti awali aliamini kuwa, jeraha hilo ni dogo na linaweza kumfanya nyota wake arejee uwanjani baada ya wiki chache.

Hata hivyo, imeripotiwa kuwa, Mbrazili huyo atakosekana uwanjani kwa muda mrefu zaidi ya uliotarajiwa.

Jarida la El Chiringuito kutoka Hispania, limeripoti kuwa, jeraha alilopata nyota huyo ni kubwa zaidi ya ilivyotarajiwa awali na anaweza kukosekana kwa wiki nne hadi sita.

Kutokana na ripoti hiyo, Real Madrid itamkosa Vinicius katika mechi kadhaa ikiwerno dhidi ya hasimu wao Atletico Madrid itakayochezwa Septemba 24, mwaka huu.

Mechi nyingine anazotarajiwakukosa nyota huyo ni dhidi ya Getafe na Real Sociedad.

Max Nzengeli afichua siri nzito Young Africans
Hifadhi ya Kitulo yapigiwa chapuo kuwavutia Watalii