Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Vinicius Junior anafanya bidii binafsi kuharakisha kupona kutoka kwenye jeraha la misuli ya paja na kurejea uwanjani kabla ya muda uliopangwa.
Vinicius aliumia katikati ya kipindi cha kwanza cha ushindi wa 1-0 dhidi ya Celta Vigo Agosti 25, mwaka huu na akalazimika kuwa nje ya dimba baada ya vipimo kuthibitisha alikuwa ameumia msuli wake wa paja la kulia.
Alitarajiwa kukosa kucheza kwa angalau majuma, lakini gazeti la Marca limesema kuna matumaini yanayoongezeka huko Madrid, Vinicius anaweza kurejea haraka kuliko ilivyotarajiwa.
Madaktari wa klabu wanafahamika kuona mechi ya dabi ya Madrid dhidi ya Atletico, ambayo imepangwa kuchezwa Septemba 24, mwaka huu kama tarehe ya kweli ya kurudi kwa Vinicius.
Uchunguzi umefanywa kila siku tangu Vinicius alipoondoka uwanjani kwa mara ya kwanza na wanaohusika wanasema maendeleo yake ni mazuri.
Jeraha hilo liliongeza kile ambacho kimekuwa mwanzo mgumu kwa kampeni ya sasa ya Vinicius, ambaye alikuwa akizoea maisha katika jukumu jipya uwanjani.
Kuondoka kwa Karim Benzema na baadaye kusajiliwa kwa kiungo Jude Bellingham kumemfanya Kocha, Carlo Ancelotti kuachana na mfumo wa 4-3-3 ambao ulifanya maajabu kwa Vinicius na kupendelea 4-1-2-1-2 ili kuongeza mchango kwa raia huyo wa England.