Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Vinícius José Paixão de Oliveira Júnior, anajiandaa kuanza mazungumzo na Uongozi wa Real Madrid kwa lengo la kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya mjini Madrid-Hispania.

Vinicius Junior ambaye alijiunga na Real Madrid mwaka 2018 akitokea klabu ya Flamengo ya nchini kwao Brazil, bado amebakiza miaka minne kumaliza mkataba wake, lakini ripoti ya gazeti la Marca imedai kuwa, kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji watano wanaolipwa mishahara midogo zaidi licha ya umuhimu wake.

Vinicius mwenye umri wa miaka 21, anakadiriwa kukusanya kiasi cha euro milioni 4 kwa msimu kulingana na makataba wake wa sasa, alifunga mabao mawili dhidi ya Elche, Jumamosi (Oktoba 30), wakati vijana hao wa Carlo Ancelotti wakishinda mabao 2-1 kwenye mchezo wa La Liga.

Mchezaji huyo amefunga mabao 23 na asisti 28 kwenye michezo 132 akiwa Real Madrid tangu ahamie kutoka Flamengo, Julai mwaka 2018.

Jay Z ajiunga tena na Instagram
Juventus kumrudisha Paul Pogba