Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania DPP Biswalo Mganga amewafutia mashtaka yaliyokuwa yanawakabili Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, BAVICHA Nusrat Hanje na Mratibu wa Uhamasishaji wa Baraza hilo Twaha Mwaipaya na wenzao sita katika Mahakama ya Mkoa wa Singida.

Wanasiasa hao wameachiwa huru usiku wa Novemba 23,2020 baada ya kusota rumande mkoani Singida kwa takribani siku 170.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye ukurasa wa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) watuhumiwa hao waliachiwa siku ya jana tarehe 23/11/2020 usiku huku wakitaja sababu yakuachiwa kuwa  upande wa Jamhuri  haupo tayari kuendelea na kesi hiyo.

Nusrat Hanje, Mwaipaya pamoja na wenzao sita walikuwa wanakabiliwa na  tuhuma zakufanya mikusanyiko isiyo ya halali , kudharua wimbo na bendera ya taifa .

Aidha kwa mujibu wa taarifa ya CHADEMA wanasiasa hao wanaachiwa huru wakiwa wametimiza siku 133 Gerezani huku  wakiachiwa huru kabla ya maamuzi ya rufaa yao ambayo ilitakiwa isikilizwe tarehe 25/11/2020.

CAF wapeleka fainali Misri
Nyota ya Grealish yaangaza Manchester City

Comments

comments