Vongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema) wamepanga kusherekea sikukuu ya Pasaka Gerezani mara baada ya Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe kuwekwa mahabusu.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalumu wa Chama hicho, Anatropia Theonist, ambapo amesema kuwa viongozi wa Chadema watakwenda kusherekea Pasaka Gerezani.

Amesema kuwa kuendelea kuwepo Mahabusu kwa Mwenyekiti wa Chama hicho kimewafanya viongozi wengi wa Chama hicho kwenda kusherekea sikukuu ya Pasaka Gerezani.

“Tutawabebea zawadi za Pasaka ikiwemo vyakula viongozi wetu hawa, tutaanzia Gereza la Segerea baada ya kuwaona kila mmoja ataenda kwake kumalizia sherehe,”amesema Anatropia

Aidha, amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na viongozi wengi wa chama hicho kuwekwa rumande hivyo, njia bora ya kuwafariji ni kuwatembelea.

UKAWA waituhumu serikali kwa hujuma

 

 

Video: Viongozi Chadema wahamia Gerezani, Nyundo za Maaskofu Zaitesa Serikali
Netanyahu apongeza jeshi lake kuwaua Wapalestina