Mkutano wa kilele wa kundi la Mataifa tajiri na yaliyoendelea zaidi kiviwanda la G7 umeanza katika mji wa mwambao wa Cornwall nchini Uingereza, huku janga la virusi vya corona likitarajiwa kugubika mazungumzo hayo ya siku tatu. 

Sehemu ya viongozi wa wakuu wa Mataifa ya kundi hilo wamewasili kwenye hoteli ya Carbis Bay iliyo kwenye fukwe za mji wa Cornwall kwa mkutano huo wa G7 utakaojaribu kutafuta majibu kuhusu janga la corona

Aidha Rais wa Marekani Joe Biden na mwenyeji wake Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson walikuwepo mjini humo tangu Jumatano na jana walikuwa na mazungumzo mapana kuhusu ushirikiano kati ya Washington na London.

Viongozi wa nchi hizo maarufu kama G7 tayari wameshaahidi kutoa msaada wa dozi bilioni moja za chanjo kwa nchi zinazoendelea, ili kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.

Nchi hizo saba ni pamoja na Marekani, Ujerumani, mwenyeji wa mkutano huo Uingereza na Canada.

Nchi nyingine ni Ufaransa, Japan na Italia. Viongozi kutoka Korea Kusini, Afrika Kusini na Australia pia wanashiriki kwenye mkutano huo na India pia itashiriki lakini kwa njia ya video.

Askari elfu 34 kupandishwa vyeo
Jaji Mkuu Mahakama ya Kenya asisitiza majaji kuteuliwa