Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na viongozi wa vyama vingine viwili vinavyounda Serikali ya mseto walifanya mazungumzo ya dharura kujadili hatma ya mkuu wa shirika la ujasusi wa nchi hiyo, Hans-Georg Maassen

Maassen anashinikizwa ajiuzulu tangu alipotoa kauli kuwa Serikali ilikuwa inasambaza taarifa zisizo za kweli kuhusu ghasia zinazodaiwa kufanywa na wafuasi wa makundi ya mrengo wa kulia dhidi ya wageni mashariki mwa Ujerumani.

SPD imesema msimamo wao ni wazi kuwa wanamtaka Merkel kumfukuza kazi Maassen, lakini Waziri wa Mambo ya Ndani, Horst Seehorfer anayeongoza chama cha Christian Social Union – CSU, amesema ana imani na utendaji kazi wa Maassen na hivyo haoni sababu ya kumfuta kazi.

Aidha, baada ya mazungumzo yaliyodumu kwa dakika 90 kati ya Merkel, kiongozi wa SPD, Andrea Nahles na Seehofer hakuna muafaka ulioafikiwa ambapo viongozi hao watakutana tena na uamuzi unatarajiwa kutolewa Jumanne wiki ijayo.

Hata hivyo, hayo yanakuja huku ikidaiwa kuwa mkuu huyo wa shirika la Ujasusi alitoa taarifa nyeti za kijasusi kwa chama chenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia ‘Alternative für Deutschland’ AfD.

CUF waiwekea ngumu Chadema, wasema hang’oki mtu
Video: CCM yalia kuchezewa rafu na Chadema