Viongozi wa Afrika wametakiwa kuungana na kuwa na kauli moja katika juhudi za kukabiliana na maendeleo ya uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini unaolikumba bara hilo.

Akizungumza katika siku ya pili ya mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa katika Mji Mkuu wa Kenya, Nairobi, Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesisitiza umuhimu wa uwepo wa kauli moja katika kufanikisha jitihada hizo.

Mkutano huo, ambao umehudhuriwa na marais wasiopungua kumi na watano kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ulijadili mchango wa nchi zao katika ufanikishaji wa nguvu za pamoja, ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Amesema, ili kupata suluhu zinazohusu mwitikio wa juhudi za kukabiliana na maendeleo ya uchumi, mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini barani Afrika, viongozi hawafai kujitenga.

Mwenyeji wa mkutano huo, Rais William Ruto, kwa mara nyingine ameulalamikia mfumo wa kifedha wa ulimwengu usio na usawa, na kutoa wito wa kufanyika mabadiliko muhimu.

Hata hivyo, Wakuu hao wa nchi pia wamejadili ufadhili unaohitajika ili kuimarisha nguvu za kijamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko hayo, pamoja na mishtuko mingine inayohusiana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Gamondi awaonya Maxi, Aziz Ki, Mkude
Mayele: Huyu Maxi ni moto wa kuotea mbali