Baraza la makanisa ya Pentekoste Tanzania (CPCT) mkoa wa Morogoro wameungana na jitihada za Serikali ya Mkoa huo kwa kutoa kiasi cha shilingi milioni moja za kitanzania ikiwa ni mchango wao katika kupambana na ugonjwa wa CORONA mkoani humo.
Wakati akipokea fedha hizo mkuu wa mkoa huo Loata Ole Sanare amewashukuru viongozi hao kwa mchango walioutoa na kusisitiza kutoa elimu kwa watu wanao wanaowahudumia katika maeneo yao jinsi ya kujiinga na maambukizi ya virusi vya Corona.
Hivi karibuni RC Sanare alifanya kikao na wadau lengo ikiwa ni kukusanya michango mbalimbali ambapo ahadi walizotoa siku ya kikao pekee fedha na vifaa vyote vikiwa na jumla ya zaidi ya shilingi 141Mil.
Wakizungumzia mara baada ya kutoa msaada huo, Viongozi wa CPCT wakiongozwa na Askofu Bryson Msuya Askofu wa TAG Morogoro Kaskazini ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa CPCT Mkoa wa Morogoro ameeleza kuwa wameguswa na jitihada za Mkuu wa Mkoa za kupambana na ugonjwa wa corona