Viongozi wa dini nchini wamekemea vitendo vya vurugu wakati nchi ikelekea katika uchaguzi mkuu utakaofanyika jumatano ya Agosti 28,2020.

Hayo yamesema na Askofu Jackson Sosthenes wa kanisa la Anglikana dayosisi ya Dar es Salaam katika mkutano wa viongozi wa dini kuelekea uchaguzi mkuu.

”Tunasihi ushirikiano wa vyama vyote vya siasa kutanguliza uzalendo wa nchi yetu kwanza na maslahi mapana ya taifa letu, sote kwa pamoja tukemee na kuhamasisha wafuasi wetu kuondokana na vitendo vyote vyenye kuashiria uvyunjaji wa amani”.amesema Askofu Sosthenes.

”ugomvi, matusi na kejeli hayo yote sio utamaduni wetu tuendeleze utamaduni wetu wa kushindana kwa hoja yunasisitiza na kivisihi vyama vya siasa kuhimiza watanzania pasipokujali itikadi zetu tufahamu Tanzania yetu inadhamani zaidi kuliko tofauti zetu” amesema Askofu Sosthenes.

Mchakato wa Uchaguzi mkuu wa Rais na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Znzibar Ubunge, uwakilishi na udiwani unaendelea, ambapo kwa sasa timu ya taifa ya uchaguzi (NEC) imeanza kutoa fomu za kugombea nafasi hizo.

Kamanda wa Polisi Morogoro afunguka ajali ya contena kukandamiza gari
Kashembe: Tunasajili kiufundi, hatukurupuki