Viongozi wa kidini wamekutana na Kiongozi wa Kijeshi wa Niger na Mkuu wa Serikali ya Kijeshi, Jenerali Abdourahamane Tchiani ambaye amewaambia yuko tayari kwa mazungumzo ya kidiplomasia na Viongozi wa Jumuiya ya kikanda wa ECOWAS.
Kauli hiyo, inafuatia mizozo kadhaa na Wajumbe hao wa Kimataifa, waliojaribu kupatanisha mzozo wa kisiasa nchini humo, na ambao walishuhudia Mapinduzi ya Kijeshi yaliyomuondoa madarakani Rais wa Niger, Mohamed Bazoum Julai, 2023.
Viongozi wa kidini wa Nigeria wakiongozwa na Sheikh Abdullahi Bala Lau, Kiongozi wa Harakati, Izala Salafist, dhehebu la Kiislamu ndio walikutana na Viongozi wa Mapinduzi Agosti 12, 2023 baada ya kuidhinishwa na Rais wa Nigeria na Mwenyekiti wa ECOWAS, Bola Tinubu.
Taarifa ya Baba Lau inasema, Jenerali Tchiani pia aliomba radhi kwa kuwaepuka wajumbe wa awali wa ECOWAS akisema alikuwa na hasira na uchungu kwamba ECOWAS ilitoa amri ya kurejeshwa rais Bazoum bila kuwasikiliza na kuona kwamba inapendelea upande mmoja pekee.