Mashetani wekundu (Man Utd), bado wamekomalia dili la kutaka kumng’oa nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambapo sasa kocha Louis Van Gaal ameweka mezani mkwanja wa pauni million  90.

Jeuri hiyo ya Van Gaal si yake pekee yake, bali inapewa baraka na uongozi mzima wa Mashetani hao.

Taarifa za ndani ya Old Trafford zinasema kuwa, uongozi wa klabu hiyo uliitana katika jiji la Los Angeles nchini Marekani kujadiliana juu ya usajili wa dirisha la Januari ambapo kikao hicho kilihudhuriwa pia na Louis Van Gaal.

Habari za kimtandao zinasema kuwa Van Gaal aliambiwa ukweli kuwa, lazima timu isajili wachezaji wa maana kwa ajili ya kuipa mataji United, na wakamwambia asiwe na wasiwasi juu ya usajili huo, hata kama atamuhitajika Cristiano Ronaldo.

Katika namna ya kuonyesha jeuri ya fedha, meneja huyo aliambiwa kama anataka kumsajili nyota huyo wa zamani wa United, wao kama vingozi wametenga mkwanja wa kutosha, lakini kwa sasa wameweka mezani pauni 90 za kuanzia.

Taarifa za United kuongeza mbio kwa ajili ya Ronaldo inakuja siku chache baada ya mshambuliaji huyo kutamka bayana kuwa, katika soka lolote linaweza kutokea na kwamba yuko tayari kuihama Real Madrid iwapo muda wa kufanya hivyo utafika.

Cristiano Ronaldo aliingia katika rada za United katika kila kipindi cha usajili, ikiwemo kile cha mwaka 2013 ambapo Mashetani hao Wekundu walikaribia kumnasa nyota huyo aliyewahi kutamba akiwa Old Trafford chini ya meneja Alex Ferguson.

Louis Van Gaal, amenukuliwa akisema, bado anapambana kwa ajili ya kumnasa Ronaldo na tayari klabu imeshamtengea pauni million 90 za kutua Old Trafford.

“Kila timu kubwa ina malengo ya mchezaji kama Cristiano, ni straika aliye katika kiwango bora licha ya ukweli kwamba ana mkataba Real Madrid, lakini hilo halizuii harakati za United kusaka saini ya kumrejesha tena Old Trafford,” alisisitiza Van Gaal kwa uhakika zaidi.

Hiddink Bado Ana Matumaini Makubwa Na Chelsea
Esther Bulaya Am-mwaga Wassira Mahakamani