Uongozi wa uwanja wa taifa wa Uingereza, Wembley umekanusha taarifa za kupokea ofa ya Chelsea ili klabu hiyo iweze kuutumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani.

Uongozi wa uwanja huo umekanusha taarifa hizo kufuatia baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa klabu ya Chelsea imewasilisha kitita cha paund milioni 11.

Chelsea, wameripotiwa kufanya hivyo ili kupata sehemu ya uwanja wao wa nyumbani kufuatia uwanja wao wa sasa wa Stamford Bridge, kuwa katika mchakato wa kufanyiwa maboresho.

Taarifa kutoka kwenye uongozi wa uwanja wa Wembley zinaeleza kuwa, hakuna ofa yoyote iliyowasilishwa kwao na wameshtushwa kusikia vyombo vya habari vikiripoti taarifa ambayo haikuthibitishwa na wahusika.

Chelsea haitokua klabu ya kwanza kutaka kubadili uwanja wake wa nyumbani kwa dharura, klabu kama West Ham Utd pamoja na Tottenham Hotspurs zimeshawahi kufanya hivyo kwa kutaka kuutumia uwanja wa Olympic wa jijini London kwa lengo la kupisha maboresho kwenye viwanja vyao.

Chelsea Yazipiga Kanzu Klabu Nguli Barani Ulaya
Udhalilishaji Wamnyima Ulaji Uwanjani