Mbunge, Shamsi Vuai Nahodha ameitaka Serikali kuangalia namna ya kuwafunza Viongozi suala la uzalendo ili kuweza kuepuka matatizo mbalimbali ya kiutendaji na usababishaji wa hasara kwa Tifa kama ilivyoainishwa katika ripoti ya mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.

Nahodha ameyasema hayo hii leo Aprili 13, 2023 Bungeni jijini Dodoma na akaongeza kuwa suala la amaadili hutengenezwa tangu utotoni kwa kuwafundisha watoto mambo memba ambayo huwasaidia katika makuzi yao na baadaye kuwa viongozi wema.

“Tujiulize kwanini maadili haya yanaporomoka, mimi nafikiri ni kosa letu sisi wazazi. Zamani Baba wa Taifa alianzisha shule za uongozi lengo lilikuwa ni kuwafundisha watu mambo muhimu ikiwemo maadili sasa sisi tunakosea wapi kila siku matatizo yanaendelea? tunapaswa kubadilika,” amesema Nahodha.

Aidha, amesema suala la kupenda kuwaachia wadada wa kazi watoto wao bila kujua historia ya mlezi wa mtoto huyo pia lina walakini kwani huchangia kuporomoka kwa maadili na kusababisha wengi wao kukua bila malezi ya mama ambaye ana uchungu na mwanae.

Liverpool yapigwa za uso kwa Jude Bellingham
Wanne warejea kuikabili Young Africans