Afarah Suleiman – Babati, Manyara.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amewataka Viongozi Nchini kutambua ubunifu wa Vijana, ili kuwaondoa na tatizo la ajira.

Waziri Mhagana ameyasema hayo hii leo Oktoba 10, 2023 Mkoani Manyara baada ya kuzindua maonesho ya wiki ya Vijana Kitaifa mwaka 2023 kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa huku akitoa wito kwa Benki mbalimbali Nchini, kutoa mikopo ya Riba nafuu Kwa Vijana hao, ili waweze kufikia ndoto zao.

Amesema, Serikali inaendelea kuwaendeleza Vijana kwenye sekta ya Kilimo, Mifugo na uvuvi kwa kuwapa elimu ya Kilimo cha kisasa, ambapo wengi kati yao tayari wamenufaika.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Joyce Ndalichako amesema lengo la kuanzishwa kwa wiki hilo ni kuwakutanisha Vijana na kubadilishana mawazo juu ya namna ya kujiinua kiuchumi.

Awali Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga amesema Wiki ya Vijana inayofanyika Manyara, imeunufaisha Mkoa huo kwa kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa, huku Wafanyabiashara wakinufaika na fursa zilizojitokeza.

Mitaala mipya: Wizara yawatoa hofu Wamiliki Shule Binafsi
Mapigano Palestina: Miili 1,500 yapatikana