Viongozi wanne wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (CHADEMA) Kilimanjaro akiwemo Mbunge wa viti maalum, Lucy Owenya wamekamatwa na polisi kwa amri ya mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.

Lucy na viongozi wanne wamekamatwa leo Ijumaa Septemba 20, 2019 kwa tuhuma za kwenda shule ya sekondari Rundugai wilayani humo na kufanya siasa kinyume cha utaratibu.

Wengine waliokamatwa ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Hai, Helga Mchomvu, katibu wa mbunge wa Hai, Irene Lema na Diwani wa Machame Kaskazini, Clement Kwayu.

Sabaya alipozungumza na gazeti la Mwananchi amesema kuwa viongozi hao walikwenda katika shule hiyo kwa madai ya kuzungumza na wanafunzi na kutoa misaada bila mkurugenzi wa halmashauri hiyo kuwa na taarifa.

Sabaya amesema taratibu zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli akitaka kuwe na utaratibu wa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Halmashauri kuhusu misaada kuhakikisha misaada hiyo inajulikana na inaratibiwa.

Aidha, Sabaya amesema kuwa ameamua kuwachukulia hatua viongozi hao wa Chadema kwani mara kwa mara wamekuwa wakifanya hivyo bila kutoa taarifa kama ambavyo taratibu zinaelekeza.

Video: Rais Magufuli amtumbua Mkuu wa Mkoa Morogoro
Alikiba - Ni kweli mke wangu nilimrudisha kwao, wasipende kuingilia maisha ya watu