Mamlaka jijini Kigali nchini Rwanda imepiga marufuku matumizi ya vipaza sauti vinavyotumika kutoa adhana kwenye misikiti, ikidaiwa kuwa kelele hizo zinawasumbua wananchi na kuwataka viongozi wa misikiti hiyo kutafuta njia mbadala za kuwaarifu waumini wao saa za ibada bila kutumia vipaza sauti.
Agizo hilo ni kufuatia siku chache zilizopita mamlaka hiyo jijini Kigali kuyafungia makanisa zaidi ya mia saba kwa ajili ya kuzuia kelele zilizotokana na vipaza sauti wakati wa ibada na baadhi ya makanisa kufungiwa kwa kukosa usajili.
“Baada ya kutathmini tatizo la kelele zinazowasumbua wananchi wakati wa ibada makanisani iliamuliwa kwamba hata vile vipaza sauti vilivyoko juu ya misikiti ambavyo waislamu hutumia wakati wa ibada kwamba vikome” amesema Nyarugenge.
-
Video: Lissu – Mwili wangu umejaa vyuma, Mwili wa tajiri wa mabasi wakutwa kwenye kiroba
-
Video: Wajaribu kuandamana waone- Masauni
Ameongezea kuwa ”Tuliwaomba viongozi wa misikiti watafute njia mbadala za kuwataarifu waumini wao saa za ibada bila kutumia vipaza sauti kwa sababu vinasababisha kelele”.
Kwa mujibu wa maelezo ya mshauri mkuu wa mufti wa Rwanda Sheikh Mbarushimana Suleiman taarifa hiyo imepokelewa na imeanza kufanyiwa kazi.
Sheikh Suleiman amefafanua kuwa Kama vile yalivyofungwa makanisa zaidi ya mia saba wiki mbili zilizopita jijini kwa ajili ya kelele huenda hii ni ishara kwamba hata misikiti ikafuatia endapo wenyewe watashindwa kuridhia agizo hilo.
Lakini kufuatia agizo lililotolewa na mamlaka ya tarafa ya Nyarugenge mjini Kigali ambalo ni moja ya eneo lenye waislamu wengi wamesema inawezekana kuanzia sasa sauti za adhana zisisikike kwa upeo wa juu.