Mabingwa wa Soka nchini Uganda Viperes SC imefungua milango kwa Klabu yoyote ya Tanzania inayomuhitaji Kiungo wao Bobos Byaruhanga katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili.
Bobos amekua akitajwa kuwa katika mipango ya Klabu nguli za Dar es salaam Simba SC na Young Africans, huku kila mmoja akitajwa kuwa katika mazungumzo ya kumsajili.
Uongozu wa Vipres SC umesema upo tayari kuanza mazungumzo na Klabu yoyote ya Tanzania kama inamuhitaji Kiungo huyo, lakini hadi sasa hakuna chochote kinachoendelea.
Simba SC yainyima utulivu Vipers SC Ligi ya Mabingwa
Afisa Mtendaji Mkuu wa Vipers ya Uganda Simon Njuba amesema wamekua wakisikia na kuona katika Mitandao ya kijamii kuhusu Bobos, lakini hadi sasa hakuna Ofa yoyote iliyowasilishwa kwao kumuhusu kiungo huyo.
Njuba amesema wapo tayari kumuuza mchezaji huyo kwa mujibu wa mkataba uliopo kati yake na Uongozi wa Vipers SC, hivyo Klabu inayomuhitaji inakaribisha kubisha hodi nchini Uganda.
Kuhusu Young Africans kuwa katika nafasi nzuri ya kumsajili, kiongozi huyo amesema suala hilo sio la kweli, huku akisisitiza yoyote atakayewasilisha ofa nzuri atamsajili Bobos, katika kipindi hiki ama mwishoni mwa msimu huu.
“Siwezi kuzungumzia chochote kwa sababu Yanga hawajaleta ofa mezani na siwezi kusema mchezaji anauzwa ama laa, lakini timu inayomuhitaji waje menzani tuzungumze, kipingele cha mkataba wake kinanizuia kusema ana mkataba wa muda gani” amesema Njuba
Simba SC, Young Africans na Klabu zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zipo kwenye mchakato wa kuboresha vikosi vyao katika kipindi hiki, baada ya kufunguliwa kwa Dirisha Dogo la Usajili Desemba 16 na kufungwa rasmi Januari 15-2023.