Shirika la viwango Tanzania TBS kanda ya kaskazini limeteketeza bidhaa mbalimbali zikiwemo vipodozi ambavyo vimepigwa marufuku vyenye thamani ya shilingi milioni 70 ambavyo vimekamatwa baada ya maofisa wa shirika hilo kufanya ukaguzi katika Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro Manyara na Tanga.
Mkaguzi kutoka TBS William Mhina akizungumza jijini Arusha baada ya kuteketeza bidhaa hizo zenye uzito wa tani moja amesema ukaguzi huo umefanyika katika maduka mbalimbali ya vipodozi kwenye mikoa hiyo.
Baada ya uteketezaji wa bidhaa hizo Mhina ameendelea kuwaonya wafanyabiashara kuzingatia sheria inayopiga marufuku uuzaji,usambazji na uhifadhi wa bidhaa hizo ambazo zimepigwa maruku na zina athari kubwa endapo zitatumiwa na binadamu.