Klabu ya Soka ya Simba imepoteza mchezo wake wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara baada ya kufungwa kwa mabao 2 – 1 dhidi ya Kagera Sugar kwenye mchezo uliopgiwa Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Kagera ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata mabao mawili ya haraka kunako kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake, Kassim Khamis dakika 17, kabla ya bao la pili kufungwa na Ramadhani Kapera dakika 41, na kupelekea mpaka mapumziko Simba wakiwa nyuma.

Kupitia Mshambuliaji wake wa kimataifa, Emmanuel Okwi Simba walipata bao la kufutia machozi dakika ya 67, na kupelekea mpaka mwisho wa mchezo huo Simba wakipoteza alama 3 muhimuambazo zingeweza kuwasogeza mbele.

Kwa matokeo hayo sasa Simba wanaendelea kusalia na alama 60 wakiwa wamecheza michezo 23, huku ligi ikiongozwa na Mabingwa wa zamani Klabu ya Yanga kwa alama 74 lakini wenyewe wakiwa wamecheza michezo 32, huku Azam FC wakishika namba mbili kwa alama 66.

Wananchi mkoani Njombe wamtosa kiongozi wao, 'Tatizo hapa ni siasa'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Aprili 21, 2019